Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili Judith Amoni
Mwansansu (39) Mkazi wa Mwanjelwa na Aive Alex Swalo (17) Mkazi wa
Mwanjelwa Mtaa wa Soko kwa kosa la kumfanyia vitendo vya ukatili mtoto
aitwaye Daines Kefas Mwansasu (06) Mwanafunzi wa Shule ya Awali –
Mlimani na Mkazi wa Mtaa wa Soko hapa Jijini humo.
Taarifa ya tukio hilo imetolewa jana tarehe 1 Agosti, 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Ulrich Matei.
Akielezea
kuhusu tukio hilo kwa wanahabari, Kamanda Matei amesema tukio hilo
lilifanyika Jumanne majira ya saa tatu usiku ambapo jeshi la polisi
lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa raia wema, ya kwamba mtoto
huyo amejeruhiwa sehemu mbalimbali kwa moto.
“Inadaiwa
kuwa siku hiyo ya tukio mhanga alikuwa ameenda kucheza na rafiki zake
na aliporudi nyumbani majira ya jioni ndipo shangazi yake alimuadhibu
kwa kumchapa na waya wa umeme sehemu mbalimbali za mwili wake na
kumsababishia majeraha na maumivu makali mwilini. Inadaiwa kuwa tarehe
01.08.2018 majira ya asubuhi, watuhumiwa waliendelea kumfanyia vitendo
vya ukatili mtoto huyo kwa kumuunguza kwa moto sehemu za miguuni na
kwenye makalio,” ameeleza Kanada Matei.
Kamanda
Matei amesema kuwa “Mtoto amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake
baada ya kufanyiwa vitendo vya ukatili na shangazi yake akishirikiana na
mtoto wake. Watuhumiwa wote wawili wamekamatwa kwa mahojiano zaidi
kuhusiana na tukio hilo. Mhanga amelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya
kwa matibabu zaidi ya kitabibu.”
Katika
hatua nyingine, amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea
kukabiliana na vitendo vya uhalifu na ajali za barabarani ili
kuhakikisha kuwa wageni na wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na
mali zao.
“Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kushirikiana na wananchi na
wadau wengine wa usalama hali inayopelekea kupata mafanikio makubwa
ikiwa ni pamoja na kupungua kwa matukio makubwa ya uhalifu pamoja na
ajali za barabarani,” amesema.
Kamanda
Matei ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa
Jeshi la Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahalifu.
Pamoja na kwa wazazi/walezi kujiepusha na vitendo vya ukatili na
unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wao kwani ni kinyume cha sheria.
Mpekuzi.
Comments