Waziri
wa Madini Angellah Kairuki amesema Serikali itaaendelea kusimamia
ulinzi na kudhibiti utoroshaji wa madini ya Tanzanite na watakaokwenda
kinyume na matakwa ya Sheria, kiama chao kinakuja.
Waziri
Kairuki aliyasema hayo tarehe 1 Agosti wakati wa ziara yake mkoani
Manyara wakati alipotembelea migodi mbalimbali ya madini ya tanzanite
ndani ya ukuta wa Mirerani.
Alisema
ziara hiyo ililenga kuangalia suala zima la ulinzi katika ukuta
unaozunguka migodi ya tanzanite, shughuli za uchimbaji madini mengine
zinavyofanyika na kuangalia namna uzalishaji wa madini ya tanzanite
unavyoendelea katika migodi husika.
Kairuki
aliongeza kuwa, ziara hiyo ililenga kuangalia namna Sheria ya Madini
inavyotekelezwa, masuala ya Mikataba ya watumishi katika migodi na
namna migodi husika inavyolipa kodi mbalimbali za Serikali yakiwemo
masuala ya usalama sehemu za kazi na wafanyakazi kwa ujumla.
“Utoroshaji
madini hausaidii, fedha ni za haraka lakini zinawaadhibu watanzania
walio wengi kwa kuwa, fedha hizo hizo zingeweza kutumika katika miradi
mingine ya maendeleo. Hivyo, kila mtanzania awe mlizi wa mwenzake,”
alisema Kairuki.
Awali,
akizungumza katika eneo Lemshuku kunakofanyika shughuli za uchimbaji
wa madini ya Green Garnet, waziri Kairuki alisema kuwa, serikali
inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika kuchangia pato la taifa
kupitia shughuli za uchimbaji, hivyo akawaasa wachimbaji nchini kufuata
Sheria, kanuni na taratibu ili kufanya shughuli halali ikiwemo kulipa
kodi stahiki.
Akizungmzia
suala la ruzuku kwa wachimbaji wadogo, waziri Kairuki alisema hivi sasa
serikali imesitisha kwa muda utoaji rukuzu kwa kuwa inaandaa utaratibu
wa wazi na endelevu ambao utawezesha wachimbaji na serikali kunufaika
kupitia rasilimali madini.
Aliongeza
kuwa, serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa shughuli za
uchimbaji mdogo wa madini ikiwemo kuhakikisha kuwa inawawezesha
wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo kwenda katika uchimbaji wa kati na
kuongeza, “ tayari tumetenga maeneo zaidi ya 44 kwa ajili ya wachimbaji
wadogo.
Akitolea
ufafanuzi suala la vibarua katika migodi ya madini, aliwataka wale wote
wanaofanya vibarua katika maeneo hayo kuhakikisha kuwa, wanapata
mikataba yao kabla ya kuanza kazi.
Kuhusu
masuala ya utoaji leseni za uchimbaji madini, Waziri Kairuki alisema
ndani ya kipindi cha wiki 2 Tume ya Madini itaanza kutoa leseni kwa
waombaji waliokidhi vigezo na kuongeza kuwa, kwa wanaomiliki leseni bila
kuziendeleza watanyang’nywa na hivyo akawaasa wamiliki wasiokuwa na
uwezo wa kuendeleza maeneo yao kutoa tarifa ili waweze kuunganishwa na
wenye uwezo wa kuwekeza waweze kushirikiana.
Pia,
waziri Kairuki alihamasisha kuhusu uwekezaji katika mashine za kukata
na kunga’risha madini ili kuwezesha shughuli hizo kufanyika nchini na
kuongeza kuwa, kupitia Sheria Mpya ya Madini hairuhusu yoyote
kusafirisha madini ghafi nje ya nchi.
Kwa
upande wake, Kamishna wa Madini, Mhandisi David Mlabwa, alisema ni
lazima Sheria, Kanuni na taratibu zizingatiwe wakati wa utekelezaji
shughuli za uchimbaji madini na kuongeza kuwa, serikali inatambua
mchango wa kila aina ya madini yanayopatikana nchini.
Naye,
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Tumaini Magesa ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Kiteto alisema kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo la
Mirerani zinaendelea na hivyo serikali itaendelea kuboresha ulinzi na
kuhakikisha kwamba unaimalika.
Mpekuzi.
Comments