Wanakijiji 68 Watiwa Mbaroni kwa Kuharibu Miundo Mbinu......Ni Wale Ambao RC Mbeya Aliagiza Wakamatwe.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu 68 kati yao 62 ni wanaume
na 06 ni wanawake kwa tuhuma za kufanya uharibifu wa miundombinu ya maji
huko katika Kijiji cha Ngole kilichopo Kata ya Ilungu, Tarafa ya
Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Katika
msako mkali uliofanywa mnamo tarehe 17.08.2018 kuanzia majira ya saa
10:00 asubuhi hadi saa 18:00 jioni huko katika Kijiji cha Ngole jumla ya
watuhumiwa 68 walikamatwa.
Awali
mnamo tarehe 14.08.2018 kuanzia majira ya saa 10:00 asubuhi huko katika
Kijiji cha Ngole, Kata ya Ilungu, Tarafa ya Tembela watuhumiwa hao kwa
makusudi na bila halali waliharibu mabomba na vyanzo vya maji kwa
kutumia silaha za jadi na kusababisha hasara ya takribani Shilingi
Milioni 14 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwa ni
michango ya baadhi ya wanakijiji na wafadhili.
Watuhumiwa hao watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa
Polisi ULRICH MATEI anatoa msisitizo kwa watanzania na wana Mbeya wote
kuhakikisha wanalinda rasilimali zetu zikiwemo miundombinu ya afya,
elimu, barabara, maji na nishati ili kufikia malengo tarajiwa ya uchumi
wa viwanda.
Pia
Kamanda MATEI anatoa rai yeyote atakayeharibu miundombinu hiyo Polisi
tutamkamata na kumfungulia shitaka la kuhujumu uchumi [Sabotage] na
kuhakikisha wanafikishwa Mahakamani.
Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na Operesheni mbalimbali,
doria katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha hali ya Mkoa inakuwa
shwari ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa magari, kuwapima kilevi
madereva pamoja na kuendelea kutoa elimu ya matumizi salama ya barabara
kwa makundi mbalimbali ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
Mpekuzi.
Comments