Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ameruhusiwa kutoka hospitalini alipolazwa kuanzia sasa ataishi nyumbani.
Tangu
Septemba 7 mwaka jana aliposhambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 jijini
Dodoma, Lissu amekuwa akiishi hospitalini kwa matibabu zaidi.
Ujumbe
wa Lissu alioutoa jana Agosti 7, 2018ulisema; “Hello Friends of Me!!!
Good afternoon to y'all. Kwa mara nyingine nawaleteeni habari njema."
Alisema
alfajiri ya Januari 6, 2018 aliondoka Hospitali ya Nairobi nchini
Kenya na kusafiri hadi Leuven nchini Ubelgiji, kwa ajili ya matibabu
zaidi.
Lissu alisema Agosti 6, 2018 alitimiza miezi saba tangu alipowasili nchini humo.
“Agosti 7 ni miezi 11 toka siku niliposhambuliwa na watu wanaojulikana sana kama 'watu wasiojulikana.'"
"Septemba
7 mwaka jana sikulala nyumbani kwangu. Agosti 7 ya leo, miezi 11 kamili
baadae, nimeamkia nyumbani kwangu," alisema Lissu.
Aliongeza:
"Septemba 7 iliyopita wote mlikuwa na hofu kubwa kama ningemaliza siku
hiyo au siku chache zilizofuata, nikiwa hai. Miezi 11 kamili baadae,
Professor Dk Wilhelmus Jan Mertsemakers, daktari wangu tangu nilipokuja
University Hospital Leuven, amesema sina sababu ya kitabibu ya kuendelea
kukaa hospitali."
"Profesa
Mertsemakers amesema nitaendelea na uponyaji nikiwa nyumbani kwangu.
Nitatembelewa na wauguzi kila siku nyumbani kuniangalia naendeleaje. Na
nitarudi hospitali kumwona kila baada ya wiki mbili," alisema Lissu.
Katika ujumbe huo, Lissu aliendelea kusema, bado ana chuma kubwa kwenye paja .
“Liko
kama antenna ya TV za mwaka '47 na Profesa Mertsemakers amesema nitakaa
nalo kwa si chini ya miezi sita. Lakini habari ya mujini ndio hiyo:
nimetoka hospitalini."alisema na kuongeza;
"Hongereni
sana kwa kazi nzuri ya kuniuguza na kuniponya na chochote mtakachokula
au kunywa siku ya leo mnibakishie. Siko mbali."
Mpekuzi.
Comments