SERIKALI
imesikitishwa na vifo vya wanafunzi wanne ambao ni wasichana wa kidato
cha nne kutoka shule ya sekondari Kimbiji iliyopo Kigamboni jijini Dar
es salaam waliofariki kwa ajali ya maji walipokuwa wakiogelea katika
bahari ya Hindi.
Vifo
vya wanafunzi hao vilitokana na sherehe iliyoratibiwa na shule husika
ili kuwapongeza wanafunzi hao wa kidato cha nne baada ya kufanya vyema
mitihani yao ya kujipima.
Akizungumza
kwa majonzi shuleni hapo,Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amesema serikali imepokea
kwa masikitiko vifo hivyo na kutoa pole kwa wanafunzi, wazazi, na walimu
wa shule hiyo kwa msiba huo mzito.
Waziri
Jafo amewataka walimu wote nchini kujiepusha na ufanyaji wa sherehe za
wanafunzi katika mazingira hatarishi. Aidha, Waziri Jafo aliwasilisha
rambirambi kwa familia nne za wafiwa.
Wanafunzi waliofariki dunia ni Secilia Ernest Paulo, Selestina Vitus Malipesa, Agnetha Philipo Mlaki na Queen Leonard Mandala.
Mpekuzi.
Comments