Rais Magufuli Awaapisha Viongozi Aliowateua......Asema Ilimlazimu Kukaa na Majina yao Miezi Minne Akiwachuja.
Rais
John Magufuli, amewaambia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Makatibu
Wakuu alikaa na majina yao kwa muda wa miezi mine kabla ya kuwateua
kushika nafasi hizo.
Akizungumza
baada ya kuwaapisha viongozi hao leo Jumatano Agosti Mosi, Ikulu jijini
Dar es Salaam, Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kutambua ni
Mungu ndiye amewachagua.
“Nimekaa na majina yenu zaidi ya miezi minne, wengine wamepungua wengine wameongezeka.
“Tanzania
ni kubwa mno, mimi sikufaa kuwa rais, ni Mungu alitaka na ndiyo sababu
siwezi nikasimamam nikajisifu, ni Mungu alitaka vile vile Makamu wa
Rais.
“Hata
Waziri Mkuu… kwanza hata sijui nilimchaguaje, kwa sababu kuna watu
walikwenda Dodoma na suti wameshona ili wawe Waziri Mkuu, lakini
Majaliwa (Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa) ni Mungu aliamua awe Waziri
Mkuu, vivyo hivyo katika nafasi zenu,” amesema Rais Magufuli.
Aidha,
Rais Magufuli pia amesema nafasi hizo kwa viongozi hao, zimepangwa na
Mungu ambaye alitaka wazipate ambapo wakiamini hivyo kila mmoja katika
nafasi yake atatenda haki kwa wakati wake.
“Wengine
wanasema nimechagua wapinzani, nani mpinzani Tanzania hii, Kafulila
(David Kafulila, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe) mtasema ni mpinzani.
“Alipokuwa
huko alipigania suala la IPTL, akaitwa tumbili leo umteue useme umeteua
mpinzani, huyu si mpinzani ni mpiganaji wa serikali yake,” amesema.
Mpekuzi.
Comments