Naibu
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile amepiga marufuku kwa hospitali na vituo vyote vya
kutolea huduma za Afya nchini kuonesha miziki katika maeneo yote
yakutolea huduma na kuwataka kuweka jumbe zinazohusu Elimu Afya kwa umma
pindi wanapongoja kupata huduma.
Ameyasema
hayo jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua hali ya utoaji
huduma za afya katika ukumbi wa halmashauri ya Muleba katika Mkoa wa
Kagera.
"Ni marufuku kwa hospital zote kuonesha miziki katika maeneo yote ya utoaji huduma za afya" alisema Dkt Ndugulile.
Pia
Dkt. Ndugulile amemwagiza Mganga mkuu wa Wilaya ya Ngara DKt. Revokatus
Ndyekobora kuhamasisha wananchi Juu ya umuhimu wa kuudhuria kliniki kwa
mama mjamzito walau mara nne ndani ya kipindi chá ujauzito wake na
kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
"Tuongeze
kasi katika kuhamasisha wakina mama wajawazito kuhudhuria kliniki, na
kwenda kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya" alisema Dkt
Ndugulile.
Pia
alisema kuwa Serikali inaendelea kuboresha sekta ya Áfya nchini kwa
kutoa pesa ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na kuhamasisha
ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi wa vituo hivyo (Forced account)
"Miundombinu
tunaendelea kuboresha, Mkoa mzima tumeleta shilingi Bilion 5.9 kwaajili
ya kuboresha vituo vya Áfya, viwili vikiwa katika Wilaya ya Ngara
"alisema Dkt Ndugulile .
Kwa
upande mwingine Dkt Ndugulile aliendelea kusema kuwa katika kuelekea
kuboresha huduma za afya Serikali imeanzasha utaratibu wa kituo nyota
kwa vituo vya Áfya, hospitali na Zahanati, na kutoa maagizo kwa
Halmashauri zote nchini kuhakikisha Asilimia 80 ya vituo vyake vyote vya
kutolea huduma za Afya havishuki chini ya nyota tatu (3)
"Serikali
imeanzisha utaratibu wa kutoa madaraja ya Ubora kwa vituo vyote vya
kutolea huduma za Afya , tunaanzia nyota sifuri kwa maana Kwamba kiwango
chako chá Ubora ni chá chini sana Mpaka nyota 5 ambacho kiwango chako
ni chá juu sana, tunataka Asilimia 80 ya Vituo vyao vyote katika kila
halmashauri visipungue nyota tatu" Alisema Dkt Ndugulile.
Mbali
na hayo Dkt Ndugulile amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Ngara. Luten....
Kuimarisha usimamizi katika ngazi zote za Wilaya ili kuweza kufikia
Ubora wa huduma za afya kwa Asilimia 80 katika vituo vyake vyote.
Nae
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngara Dkt Revokatus Ndyekobora amesema kuwa
lishe duni kwa watoto hasa walio chini ya Miaka 5 bado imekuwa tatizo na
kusema kuwa wameweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya
tatizo lá lishe duni.
"Hali
ya Lishe bado ni shida, ambapo tunaendelea kupambana nayo na tayari
tumeweka mikakati thabiti yakuweza kupambana dhidi ya lishe duni "
alisema
DKt.
Revokatus Ndyekobora aliendelea kusema kuwa Wilaya ya Ngara ináupungufu
wa watumishi kwa Asilimia 59.2 jambo linaloleta changamoto katika
utoaji wa huduma za afya.
"Tuna
upungufu wa watumishi kwa Asilimia 59.2 , Kwaiyo tunafanya kazi katika
hali ya upungufu, tunamshukuru tumepata watumishi 36, lakini waliripoti
33, na juzi TAMISEMI waliondoa watumishi 2" alisema Dkt Revokatus
Ndyekobora
Mpekuzi.
Comments