Diwani
wa Kata ya Vingunguti (CUF), Omary Kumbilamoto ambaye pia ni naibu meya
wa manispaa ya Ilala amejizulu uanachama wa chama hicho.
Amechukua uamuzi huo jana Julai 31, 2018 huku akieleza kuchoshwa na mgogoro wa uongozi unaoendelea ndani ya CUF.
CUF
kimekumbwa na mgogoro tangu mwaka 2016 baada ya kurejea kwa Profesa
Ibrahim Lipumba ambaye mwaka 2015 alijiuzulu uenyekiti wa chama hicho
kutokana na kutofautiana na viongozi wenzake.
Kumbilamoto
ameufananisha mgogoro huo wa CUF na mvutano wa mataifa ya Palestina na
Israel, akieleza kuwa hauna suluhu na unamfanya ashindwe kuwatumikia
ipasavyo wananchi wa Vingunguti.
Amesema
amekuwa akipewa vitisho vya kufukuzwa uanachama kwa sababu ya hatua
yake ya kuwa karibu na viongozi wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Paul Makonda.
Amesema
wakati kata ya Vingunguti ikikumbwa na mafuriko, hakuna kiongozi
yoyote wa CUF aliyekwenda kutoa msaada isipokuwa Serikali ya Mkoa wa
Dar es Salaam.
“Sikuletewa
hata kijiko na viongozi wangu wa chama lakini viongozi wa Serikali
walinisaidia. Hata hivyo, upande chama kinadai mimi ni msaliti kutokana
na ushirikiano ninaoupata,” amesema Kumbilamoto.
Amesema
wakati wowote atafanya mkutano wa hadhara wa kueleza wa wananchi wa
kata hiyo wapi atakapoelekea kwa ajili ya kufanya shughuli za kisiasa.
Credit: Mwananchina Mpekuzi.
Comments