Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia mtu mmoja, aliyejulikana kwa
jina la Prosper Lema, aliyedai kutekwa na watu wasiojulikana na kuanza
kutumia uongo kuomba fedha kwa ndugu zake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amesema, taarifa hizo za Bw.
Lema zilipatikana baada ya ndugu zake mtuhumiwa huyo kwenda katika kituo
cha polisi kirumba jijini humo kutoa taarifa ya ndugu yao kutekwa na
watu wasiojulikana Julai 18, mwaka huu baada ya kuwatumia ujumbe akiomba
fedha.
Kamanda
Msangi amesema kwamba mtuhumiwa Lema aliomba fedha zaidi ya shilingi
milioni tano kwa familia yake kwa kutuma ujumbe kwenye simu ili aweze
kuachiwa huru na watu waliomteka.
Aidha ameongeza kwamba mtuhumiwa Lema atafikishwa Mahakamani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.
Mbali
na hayo, Kamanda Msangi amewatahadharisha wananchi kuwa makini na kutoa
taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapobaini kuwepo kwa dalili
zinazofanana na hizo.
Mpekuzi.
Comments