
Pia ameiamuru Idara ya Uhamiaji Wilayani humo kumnyang'anya hati ya kusafiria meneja wa kampuni hiyo, Trevor Gifford hadi fedha hizo zitakapolipwa.
Kampuni ya Tudeley inamiliki na kuendesha mashamba ya ushirika ya chama cha msingi cha Murososangi yenye ukubwa wa ekari 2,054.
Ole
Sabaya, ametoa maagizo hayo jana Agosti 16 wakati alipofanya ziara ya
kutembelea mashamba ya kampuni hiyo huku akiwa ameambatana na kamati ya
ulinzi na usalama Wilayani Hai.
Pia aliambatana na Meneja wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wilayani Hai, Spécioza Owere.
Kabla
ya kuingia katika lango kuu la kampuni hiyo Ole Sabaya aliamuru Gifford
aitwe huku akiwa na hati yake ya kusafiria na baadaye akaingia katika
ofisi za kampuni hiyo.
Akizungumza
katika eneo la tukio, Ole Sabaya alisema kwamba ana taarifa za uhakika
kwamba kampuni hiyo imekuwa ikikwepa kulipa kodi ya serikali kwa muda
wa miaka saba hadi sasa.
Ole
Sabaya alisema kwamba kampuni hiyo imekwepa kulipa kodi ya serikali
zaidi ya Sh800 milioni ambazo ni malimbikizo ya kodi ya Mamlaka ya
Mapato nchini (TRA).
Akitoa
maagizo hayo Ole Sabaya aliliamuru jeshi la polisi Wilayani humo
kumkamata Natal na Mroso na kuwekwa mahabusu kwa saa 48 na wahakikishe
fedha hizo ambazo ni kodi ya serikali zinalipwa.
"Wewe
utaenda ndani ili uje uniambie kuna utaratibu gani wa kodi ya serikali
kulipwa na ijumaa asubuhi uwepo ofisini kwangu uniambie kodi ya serikali
italipwaje,” alisema na kuongeza:
"Chukua passport yake ya zamani na sasa nataka pésa hiyo ilipwe ndani ya siku saba na TRA niletewe maelezo hayo.”
Mara
baada ya agizo hilo maofisa wa jeshi jeshi la Polisi Wilayani humo
walimkamata Natal na Mroso na kisha kuwapéleka kwenye gari huku maofisa
wa idara ya Uhamiaji wakichukua hati ya kusafiria ya Trevor.
Kabla
ya Mroso kushikiliwa alimweleza Ole Sabaya kwamba uongozi wa kampuni
hiyo ulishawasilisha maombi mbele ya ofisi yake kuwaomba TRA wakague
hesabu na madeni ili waweze kulipa.
Mpekuzi.
Comments