Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu miaka 5 jela aliyekuwa Mhasibu wa
Chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Gryson Mnyawami baada ya
kupatikana na hatia ya kosa la wizi wa zaidi ya Shilingi Milioni 9 akiwa
mtumishi.
Hukumu
hiyo, imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega ambapo amesema upande
wa mashtaka kupitia mashahidi wake 5 wameweza kuthibitisha pasipo kuacha
shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa la wizi.
Hata
hivyo, kabla ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Hakimu Mtega alitaka mwendesha
mashtaka kueleza kuhusu kumbukumbu za mshtakiwa kama anamakosa mengine
ama la.
Mwendesha
Mashtaka, wakili wa Serikali, Janeth Magoha ameekeza kuwa hakuna
kumbukumbu za makosa kwa mshtakiwa, hili ni kosa lake la kwanza.
“Sina
kumbukumbu za mshtakiwa, ila naomba mahakama itoe adhabu kali kwa kuwa
kitendo cha wizi alichofanya akiwa kama mtumishi wa umma ni kibaya,
kinaitia hasara kubwa Serikali, pia suala la wizi katika Chuo cha ustawi
limekuwa likitokea mara kwa mara Kitendo cha yeye kudhulumu wanafunzi
siyo haki kwani ile ni hela ya walipa kodi,” alisema.
Katika
utetezi wake, mshtakiwa Mnyawami, aliiomba mahakama hiyo kumpunguzia
adhabu, kwani awali alikubali kulipa fedha hizo taratibu lakini taasisi
ndiyo ilimkatalia.
“Dada yangu ni mgonjwa na mama yangu ni mjane na wote wananitegemea,”.
Katika
mashtaka yake, anadaiwa May 31, 2014 katika Chuo cha ustawi wa jamii
kilichopo Kijitonyama wilayani Kinondoni mtuhumiwa akiwa ameajiriwa kama
Mhasibu wa Chuo hicho aliiba sh, 9,714,000 mali ya muajiriwa wake
ambayo ameipata kutokana na nafasi yake kazini hapo.
Mpekuzi.
Comments