Makamu
wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amesema anashangazwa na baadhi ya
Wakurugenzi wa Halmashauri mbalimbali na wasaidizi wao kuendelea kufuja
fedha za halmashauri zao licha ya maneno mengi ya kukemea hali hiyo.
Akizungumza
baada ya kuapishwa viongozi hao Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumatano
Agosti Mosi, Mama Samia pia amewataka wakuu wa mikoa, makatibu tawala
na makatibu wakuu kufanya kazi kwa kusimamia kiapo walichoapa na
kuendeleza uhusiano mzuri kwa watakaowakuta maofisini mwao.
“Mnapokwenda huko mfanye kazi sambamba na ilani ya chama (Chama Cha Mapinduzi), hatutegemei tukizunguka hukio tukute mivutano.
“Halmashauri huko chini kuna mapato mengi ya kukusanywa lakini hayakusanywi ipasavyo na mengine yanakusanywa kinyume cha sheria.
“Mimi
nashangazwa katika halmasahuri wakurugenzi na wasaidizi wao wanafuja
fedha pamoja na yote tunayozungumza lakini bado huku chini kuna wanaume
wanafuja fedha,” amesema Mama Samia.
Pamoja
na mambo mengine, Mama Samia amewataka wakuu wa mikoa kusimamia na
kutekeleza ilani ya CCM katika kutekeleza majukumu yao.
Mpekuzi.
Comments