WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amewaonya Polisi nchini ambao
wanatumiwa na mafisadi kuwanyanyasa wananchi maskini kwa kupora ardhi
zao na kukimbilia kufungua kesi vituoni wakilazimisha ardhi hiyo iwe
mali yao.
Akizungumza
na mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha
Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa
Mara, Lugola alisema amepata malalamiko mengi kutoka sehemu mbalimbali
nchini, kuwa mafisadi uonea wananchi maskini kwa kupora kwa nguvu ardhi
wakidai wanamiliki wao na wanatumia badhi ya polisi wasiokua waaminifu
ili kuwakandamiza wananchi hao.
Kutokana
na hatua hiyo, Lugola amepiga marufuku kwa mwananchi yeyote ambaye
anakurupuka kukimbilia kituo cha polisi kufungua kesi za ardhi ambazo
hazina uthibitisho wa jinai yoyote, badala yake kesi au malalamiko yake
kwanza ayapeleke katika mabaraza ya ardhi katika eneo husika ili ziweze
kutatuliwa.
Lugola
ameongeza kuwa, mafisadi hao ambao wanafedha baada ya kuona mmiliki
halali wa ardhi hiyo anagoma kuondoka katika sehemu husika, basi utumia
fedha zake kwa kukimbilia polisi kufungua kesi bila ya kuwa na uthitisho
wowote huku baadhi ya polisi wasiokua waaminifu wakitumiwa katika
kufanikisha ardhi hiyo ananyang’anywa mwananchi huyo.
“Kuanzia
leo mwananchi yeyote atakaeenda kufungua kesi kituo cha polisi
inayohusu masuala ya ardhi na endapo kiwanja hicho kimepimwa lazima awe
na hati inayoonyesha yeye ni mmiliki halali, ili iwasaidie polisi wajue
wewe ndio mmiliki halali, na kwa upande wa ardhi ambayo haijapimwa
lazima mwananchi huyo aende polisi akiwa na uthibitisho kutoka kijijini
au katika mtaa unaosema kwamba eneo hilo ni la kwako na polisi
wathibitishe hilo,” alisema Lugola.
Lugola
aliongeza kuwa, na endapo kesi ya mlalamikaji yeyote ipo mahakamani
anapaswa kuheshimu makahama na si kuendeleza kufanya usumbufu katika
jamii pamoja na kwenda polisi na kuanza kutafuta njia ya kumsumbua
mwananchi ambaye ni maskini katika eneo hilo.
Katika
hilo, Lugola alifafanua kuwa, endapo mwananchi ana hukumu ya mahakamani
inayoonyesha ameshinda kesi hiyo, mwananchi huyo anapaswa kwenda polisi
na nakala ya hukumu yake ili polisi waweze kushuhudia kwamba pande zote
mbili ziliwahi kugombana kuhusu ardhi na kufikishana mahakamani lakini
mmojawapo alishinda.
“Rais
Magufuli alianzisha Mahakama ya mafisadi hapa nchini, kwa taarifa
niliokua nayo, mahakama hii ina uhaba wa mafisadi, sasa mimi
nitaitafutia wateja kwa kuhakikisha wale mafisadi ambao uonea wananchi,
utesa wananchi, uiba fedha za serikali au taasisi yoyote nitawafikisha
katika mahakama hiyo, hatutakubaliana na manyanyaso ya aina yoyote
katika Serikali hii ya awamu ya tano” alisema Lugola.
Lugola
aliongeza kua, hataki kusikia mwananchi anaonewa, na pia aliapa
hatacheka na mafisadi, atapambana nao sehemu yoyote nchini na pia yupo
tayari kwalolote na ameanza kupambana na mafisadi ndani ya wizara yake
na tayari wameanza kurudisha fedha za Serikali.
Aidha,
Lugola katika hotuba yake alipiga marufuku kwa waendesha bodaboda wenye
tabia ya kubeba abiria zaidi ya mmoja kuiacha tabia hiyo ili kuepusha
ajali, lakini aliwataka polisi kutorudi nyuma, wahakikishe wanawakamata
waendesha bodaboda wasiofuata sheria za usalama barabarani.
Waziri
Lugola yupo katika ziara jimboni kwake kwa kutembelea miradi mbalimbali
ya maendeleo pamoja na kuwaunganisha wananchi kupitia Bonanza lake la
michezo ya mpira wa miguu ambalo linashirikisha kila kata wakitoa
washindi mbalimbali ambao anawapa zawadi pamoja na kuingia moja kwa moja
katika mashindano ya kugombea Kombe la Kangi.
Mpekuzi.
Comments