Mwenyekiti
wa CUF anayetambuliwa na msajili wa vyama vya siasa nchini, Profesa
Ibrahim Lipumba amemtaka Maalim Seif Sharif Hamad kufuta kesi zisizo na
mashiko walizofungua mahakamani ili kuepukana na hasara ambazo zinaweza
kuepukika.
Lipumba
amesema si jambo la busara hata kidogo kwa wakati huu ambao nchi ipo
katika kipindi cha amani na utulivu kundi la watu likaibuka na kuanza
kufungua kesi za kisiasa ambazo kuwepo kwake ni kupoteza muda kwa kundi
lililofungua kesi hizo.
Lipumba
ametoa kauli hiyo jana Agosti 16 katika mkutano na waandishi na habari
huko Malindi Mjini Unguja, wenye lengo la kutoa msimamo wa chama chake
juu ya ushiriki wao katika chaguzi ndogo ndogo za wabunge na
wawakilishi, ambapo alisema kuwa chama hicho kitashiriki katika uchaguzi
mdogo wa Jimbo la Jang'ombe utakaofanyika Desemba mwaka huu.
"Hatuwezi
kuwaachia fursa ya kushiriki uchaguzi mdogo kwa kisingizio cha mgongano
uliopo baina yetu, sisi lengo letu ni kutumikia wananchi hivyo
tunaahidi kuwa tutashiriki uchaguzi bila ya wasi wasi wowote,"alisema
Lipumba.
Lipumba
aliongeza kuwa, "Niwaombe sana ndugu zangu akina Maalim Seif kufuta
kesi zao Mahakamani kwani kinyume chake wataendelea kuwanufaisha
mawakili tu wala hakutakuwa na jambo jipya juu ya kesi hizo".
Alisema
kwa kuwa CUF ni sehemu ya vyama vya siasa ambavyo vina haki ya
kushiriki uchaguzi huo wa marejeo hivyo ni wazi kuwa hawataacha
kushiriki uchaguzi ili kuwapa fursa wananchi kukichagua chao hicho ili
kuwatumikia .
Kwa
zaidi ya miaka miwili sasa, Chama cha Wananchi (CUF) kipo kwenye
mgogoro mkubwa wa kiutawala uliosababishwa na hatua ya Profesa Ibrahimu
Lipumba kujiuzulu na baadaye kutengua uamuzi huo.
Profesa
Lipumba alitangaza kujiuzulu uenyekiti, Agosti 5, 2015 lakini baada ya
mwaka mmoja akatengua uamuzi huo na kutangaza kurejea katika wadhifa huo
jambo ambalo limepingwa na baadhi ya wanachama wakiongozwa na Katibu
Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mpekuzi.
Comments