Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla anatarajiwa kuhamishiwa
katika Taasisi ya Mifupa (MoI) pindi atakapokamilisha matibabu yake
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikolazwa tangu mwishoni mwa
wiki.
Jana
akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua maendeleo ya
waziri huyo aliyepata ajali ya gari wiki iliyopita akiwa katika ziara ya
kikazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Respicious Boniface alisema kuwa
waziri huyo atahamishiwa kwenye taasisi hiyo wakati wowote. Alisema
lengo la kumhamishia kwenye taasisi hiyo ni kuendelea na matibabu ya
viungo vilivyovunjika.
Dk
Boniface alikuwa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu programu
inayoendeshwa na taasisi hiyo ya uchunguzi wa umri kwa wachezaji wa timu
ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 ambao watashiriki michuano
ya Cecafa itakayoanza jijini mwishoni mwa wiki.
Mpekuzi.
Comments