Katibu Mkuu CCM Naye Kajitosa Sakata la Ubalozi wa Marekani Kudai Uchaguzi wa Marudio Haukuwa Huru na wa Haki.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ally, ameitaka Marekani
na taasisi za kimataifa kuheshimu uhuru wa Tanzania.
Amesema
kauli iliyotolewa na Marekani kuhusu uchaguzi mdogo wa marudio
uliofanyika Agosti 12, mwaka huu katika maeneo mbalimbali nchini,
inagusa maeneo mengi na ni matarajio yake kwamba taasisi zote za nchi
zinazohusika zitazingatia madukuduku yao.
Kauli
hiyo ya Dk. Bashiru imekuja siku mbili baada ya Ubalozi wa Marekani
kutoa tamko kuhusiana na uchaguzi huo ambapo ilisema uligubikwa na
vurugu na pia haukufuata sheria.
“Nimeisoma
na nimeielewa, sisi kama chama, tunazingatia zaidi uhuru wa kitaifa
kwamba taifa hili ni taifa huru na CCM kina dhamana ya kusimamia uhuru
wa kitaifa.
“Ninachojua
mimi chaguzi zote zimefanywa kwa msingi wa sheria na matarajio yangu ni
kwamba Marekani na taasisi nyingine za kimataifa, zitaheshimu uhuru wa
taifa letu,” amesema Dk. Bashiru akihojiwa Kituo cha Deustche Welle cha
Ujerumani.
Mpekuzi.
Comments