Kamati
ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imeitaka serikali kukaa na
wamiliki wa viwanda nchini na kuhakiki gharama za uzalishaji ambazo
zimekuwa zikisababisha bidhaa za wazalishaji wa ndani kushindwa
kushindana na zinazoingizwa nchini.
Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Sadick Murad ametoa kauli hiyo jana Agosti 13, wakati
kamati hiyo ilipotembelea kiwanda cha uzalishaji wa mabati na vifaa
vingine Alaf.
Murad
amesema gharama za uzalisha zimekuwa kikwazo kwa viwanda vya ndani
ambazo vinazalisha bidhaa kwa bei ghali ilihali zinazoingizwa nchini
zinauzwa kwa bei rahisi.
“Gharama
za uzalisha zikiwa fair na wazalishaji wa ndani kupunguziwa kodi za
umeme na tozo nyingine, gharama za uzalishaji zitashuka,” amesema ambaye
pia ni Mbunge wa Mvomero (CCM).
Aidha,
alitoa wito kwa wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji, kuisimamia
vema Shirika la Viwango (TBS) na Mamlaka ya Mapato (TRA) ili ziendelee
kutoa huduma rafiki kwa wazalishaji wa ndani ambao wamekuwa chachu
katika uzalishaji wa ajira na ukuzajia uchumi.
Hata
hivyo, Katibu mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa
Joseph Buchweshaija amesema tayari imeandaa mpango maalumu wa kwa
kushirikiana na TBS kuondoa bidhaa hafifu sokoni. Tayari tumeanza
kuisafisha suala hilo na ninawaahidi kuendelea kutekeleza yote
mliyoagiza,” amesema.
Aidha,
Meneja Mkuu wa kiwanda hicho cha Alaf, Dipti Mohanty aliieleza kamati
hiyo kuwa umeme umeendelea kuwa mojawapo ya kikwazo kikubwa katika
uzalishaji wa bidhaa zao.
Mpekuzi.
Comments