Mkuu
Wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro, amewataka madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Arusha, kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza kiwango
cha ukusanyaji mapato katika halmashauri hiyo.
Muro
ameyasema hayo jana Jumamosi Agosti 11, katika Baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Arusha na kuongeza kuwa vipo vyanzo vingi vya
mapato ambayo halmashauri hiyo inaweza kukusanya hadi kufikia Sh bilioni
10.
Amesema
itafika mahala watashindwa kugharamia vikao vyao, mtashindwa kupata
posho kwa sababu hatakuwa tayari kutoa fedha badala ya kwenda kulipa
malimbikizo ya madeni ya walimu wakati wao hawatimizi wajibu wao.
“Hilo
katika uongozi wangu mtalisahau, twendeni kwa pamoja tuwasimamie wale,
tupambane, tuongeze mapato ya kutosha hata mkilipana posho wananchi
hawatatuona sisi wezi, tutasema tumelipa posho diwani ambaye anazunguka
katika maeneo yake anakagua na kusimamia maofisa tarafa na watendaji
katika kata yake.
“Lakini
wako madiwani hawajawahi hata kumsalimia sekretari wake asubuhi akiamka
hamuulizi hata Ofisa Mtendaji wake, umeamkaje, kuna nini kipya,
unaendeleaje umefuatilia ule mradi.
“Iko
miradi ya serikali mikubwa, mmeweka kwenye taarifa hapa, kuna ofisa
mtendaji hajui wajibu kwenye ule mradi ni kwenda kukagua nondo, kiwango
cha saruji kinachochanganywa, vifaa vinavyoletwa na maabara na vitu kama
hivyo,” amesema Muro.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Dk. Wilson Mahera
amesema iko baadhi ya miradi iliyokamilika na inatarajiwa kuzinduliwa na
mbio za mwenge wa uhuru wilayani humo.
Mpekuzi.
Comments