Mkurugenzi
wa habari, uenezi na uhusiano wa umma wa Chama cha Wananchi (CUF),
Abdul Kambaya amesema zaidi ya asilimia 70 ya migogoro ndani ya chama
hicho imechangiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la uongozi chama
hicho, Julius Mtatiro.
Kambaya amesema hayo ikiwa ni siku moja baada ya Mtatiro kujiengua CUF na kutangaza kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mtatiro
ambaye alikuwa upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu wa chama hicho,
Maalim Seif Sharif Hamad, alitangaza kuachana na chama hicho na kujiunga
na CCM Agosti 11, 2018.
Kambaya
amesema Mtatiro alipokuwa mwenyekiti wa mkutano mkuu alisababisha chama
hicho kugawanyika kwa kutosikiliza maoni ya wajumbe wa mkutano huo na
kuamua kuuendesha kibabe.
Ameongeza
kuwa Mtatiro alipokuwa Naibu Katibu mkuu alikiingiza chama hicho katika
mgogoro uliosababisha Hamad Rashid kufukuzwa uanachama baada ya kuhoji
ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh300milioni katika uchaguzi mdogo wa
ubunge Igunga.
“Hakuna
kitu ambacho Mtatiro amekifanya kwenye chama hiki, kubwa zaidi
amesababisha migogoro. Wanasiasa wapambanaji hawakimbii migogoro ndani
ya vyama vyao bali wanakaa humo humo mpaka migogoro itakapokwisha”
amedai Kambaya.
Kambaya
ambaye yupo upande unaomuunga mkono mwenyekiti wa chama hicho, Profesa
Ibrahim Lipumba, amesema kuwa; “Tazama Sophia Simba hakukimbia CCM
sambamba na Nape Nnauye (mbunge wa Mtama-CCM). Hata Mnyika (John-Mbunge
wa Kibamba-Chadema) hakukimbia chama hicho.”
Mpekuzi.
Comments