Jeshi
la Polisi limewakamata watu wawili wanaotuhumiwa kuiba fedha kwa njia
ya Mtandao, ambao wanatumia pikipiki yenye namba za usajili bandia MC.
759 AHW na Chassis namba PFZWFK47770 aina ya boxer.
Kamanda
aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Joseph Bakari Msinati (32) Mkazi wa
Frelimo Iringa na Elisha Athman Mdemu(35)Mkazi wa Kihesa Iringa,ambao
walitumia pikipiki hiyo kusafiri mikoa Mbalimbali mijini na vijijini
kuiba bidhaa za dukani .
“Watuhumiwa
hawa wanafika kwenye maduka na kuagiza bidhaa mbalimbali na kufanya
malipo kwa njia ya mtandao wa simu, Mara baada ya kulipa na mpokeaji
kujiridhisha kupokea fedha hiyo wanaondoka na bidhaa.
“Na
baada ya dakika chache waharifu hao wanapiga simu kwenye Kampuni namba
ya huduma kwa mteja na kudai kuwa warejeshewe fedha kwa kuwa wameituma
kimakosa, na bidhaa kwenda kuuzwa kwa watu wengine kwa bei nafuu,”
alisema Muroto.
Pia
Kamanda alisema wamefanikiwa kumkamata Daudi Charles (25) Mkazi wa
Mbagala akiwa na noti bandia 50 za shilingi elfu 10 ambazo zingekuwa
halali thamani yake ni TSH. 500,000/=.
Hata
hivyo katika tukio lingine Kamanda alisema wamekamata mali mbalimbali
za Wizi zilizotokana na matukio ya Uvunjaji na uporaji ambazo ni
Televisioni 3,Magodoro 4,Redio Subwoofer 3,Majiko ya gesi 2,Spika 3,Deck
3,mifuko ya Cement 5 pamoja na Capeti 1.
Kamanda
Muroto amewataka wananchi walioibiwa kufika polisi ili kuweza
kuzitambua mali zao, Pia aliwatahadharisha Waharifu kuwa Dodoma siyo
mahali Salama pa kufanyia uharifu.
Mpekuzi.
Comments