Waziri Mkuu Azindua Muongozo Wa Ujenzi Wa Viwanda Nchini......Pia afungua rasmi maonesho ya biashara yanayoendelea Sabasaba.
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Muongozo wa Ujenzi wa viwanda ambao
utatumiwa kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kwa lengo la kufanikisha
Tanzania ya viwanda.
Uzinduzi
wa muongozo huo wa ujenzi wa viwanda nchini ameufanya jana wakati
anafungua rasmi Maonesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
muongozo huo alisema unatoa maelekezo katika kuhakikisha ujenzi wa
viwanda unatekelezwa na kushauri wote wanaohusika na muongozo huo
kuutumia vema.
“Muongozo
wa ujenzi wa viwanda upo kwenye kijitabu hiki kidogo lakini kimefafanua
kwa kina nini maana ya kiwanda na ili kiwepo kiwanda kitu gani ambacho
kinatakiwa kufanyika.
“Kuna
dhana ambayo imejengeka kwa baadhi ya wananchi , unapozungumzia kiwanda
wanadhani labda uwe na jengo kuubwa na mashine ndani.Kumbe haiko hivyo
na kupitia muongozo huu ambao nimeuzindua leo unafafanua
vizuri,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa .
Alisisitiza
lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inatekeleza ujenzi wa
viwanda ambao utatoa fursa ya kuendelea kwa uchumi na kutoa ajira kwa
watanzania walio wengi.
Pia
alihimia ujenzi wa viwanda ambao utakwenda sambamba na viwanda ambavyo
vitatumika kuzalisha malighafi kwa ajili ya kutumia kwenye viwanda na
kwamba ili kufanikisha hilo iko haja ya kuwekeza katika sekta ya kilimo.
“Serikali
ina nia ya dhati ya kuendeleza kilimo nchini na Juni 4 mwaka huu
umefanyika uzinduzi wa mpango wa pili wa kuendeleza kilimo
nchini,”alisema.
Mpekuzi.
Comments