Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema
serikali itaendelea kushirikiana na kuimarisha uhusiano wake wa
kidiplomasia na Jamhuri ya Korea ili kuimarisha uchumi wa nchi hizo
mbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es salaam jana, Waziri Mkuu
Majaliwa akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-Yon
amesema kuwa nchi hizo mbili zimetia saini mkataba wa mahusiano ya
kidiplomasia ili kuimarisha uhusiano baina yao.
“Leo
hii tumeshuhudia utiaji saini mkataba wa kidiplomasia wa kuondoa hitaji
la visa kwa watumishi wa umma pamoja na wenye hati za kusafiria za
kidiplomasia ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wetu” amesema Waziri
Mkuu Majaliwa
Mkataba
huo wa kihistoria ulitiwa saini na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt.Agustine Mahiga, pamoja na
Makamu wa Kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Sung
Nam.
Aidha,
Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa nchi hizo mbili zitaendelea
kushirikiana ili kuimarisha maendeleo ya uchumi, utamaduni, teknolojia
ya habari na mawasiliano pamoja na sekta ya utalii.
Ameitaja
miradi mikubwa mitatu wanayotarajia kutekelezwa katika ushirikiano wan
chi hizo kuwa ni ujenzi wa daraja la Busisi lililopo Kigoma lenye urefu
wa mita 3200, ujenzi wa eneo lililobaki la barabara Cheya mkoani Tabora
lenye urefu wa km 2.
Miradi
mingine mikubwa ya ushirikiano huo ni pamoja na kuimarisha sekta ya
afya kwa kujenga hospitali tano za rufaa katika kanda mbalimbali nchini.
Sambamba
na hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Waziri Mkuu huyo wa Jamhuri
ya Korea Lee Nak- Yon amefurahishwa na amani iliyopo nchini, na
kumuahidi kuwa Tanzania itaendelea kuwaunga mkono katika mazungumzo yao
ya amani huko Korea.
Waziri
Mkuu huyo wa Jamhuri ya Korea, aliyewasili nchini jana anaendelea na
ziara yake ya siku tatu, ambapo baadae leo atatembelea kituo cha taarifa
cha NIDA kilichopo Kibaha,mkoni Pwani.
Mpekuzi.
Comments