Serikali kuimarisha kilimo cha mpunga.

WAZIRI wa Kilimo Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Rashid Ali Juma, amesema serikali itaweka mazingira wezeshi ya uzalishaji mpunga ili kutoa fursa kwa wakulima, kuongeza uzalishaji wa kilimo hicho nchini.

Hivi karibuni, gazeti hili lilichapisha makala kuhusu changamoto zinazowakabili wakulima wa mpunga, hali inayosababisha uzalishaji wa mchele kutokidhi mahitaji ya wananchi.

Makala hiyo inatokana na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya miezi mitatu katika mabonde mbali mbali ya mpungua.

Aliyasema hayo bonde la Kibokwa Wilaya Kaskazini ‘A’ wakati akizindua uvunaji mpunga kwa msimu wa mwaka huu na kuongeza kipato kwa wakulima.

Alisema serikali inachukua jitihada mbali mbali za kuimarisha kilimo cha mpunga kwa kuongeza uzalishaji wa mpunga ili kuhakikisha Zanzibar inajitegemea kwa chakula.

Aliwaomba wakulima kutumia mbinu bora za kilimo sambamba na matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo ili kuongeza uzalishaji.

Zanzibarleo.

Comments