Jeshi
la polisi mkoani Dodoma limekamata Wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia
pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao.
Akizungumza
na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoani hapa Gillis Muroto
alisema, Wahamiaji hao walikamatwa katika barabara kuu ya Dodoma
kuelekea Arusha kijiji cha Kuhi kata na tarafa ya Bereko Wilayani
Kondoa.
Kamanda
Muroto Alisema Wahamiaji hao walisafirishwa na gari lenye namba za
usajili T. 898 AHM na tela namba T. 422 ADD aina ya Scania mali ya
Kampuni ya SANVIC LTD. Watanzania waliokuwa wanawasafirisha Wahamiaji
hawa ni Dereva Julius Jackson Kitoma(57) Mnyaturu na mkazi wa Ngarenaro
Arusha, Abedi Raphael Nyomolelo (20) Utingo wa gari hilo na Mkazi wa
Sakina Arusha.
Wengine
ni Ramadhani Salumu Mawazo (39)Mzaramo pia mkulima na mkazi wa Mbagala
Dar es Salaam pamoja na Juma Ramadhani Husei (46) Mzigua, mkulima na
mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam, aliwataja Muroto.
Aidha
alisema kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu ya kuwafungia Wahamiaji hao
kwenye Contena la Mizigo, wakiwachanganya na bidhaa walizokuwa
wakizisafirisha ambazo ni maboksi yenye Vizibo vya Soda na bia kutoka
Namanga- Arusha kuelekea Mbeya.
Mpekuzi.
Comments