Wagombea 30 wa Udiwani katika uchaguzi Mdogo wa kata 77 utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu, wamepita bila kupingwa.
Akizungumza
Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC), Dkt. Athumani Kihamia amesema kuwa wagombea hao wamepita
bila kupingwa baada ya Tume kukutana, kujadili na kuyatolea maamuzi
mapingamizi mbalimbali yaliyoweka na wagombea wa udiwani.
Amesema
Madiwani wote waliopita bila kupingwa wanatoka Chama cha Mapindizi
(CCM) na kuongeza kuwa rufaa zilipokelewa na kujadiliwa kwa kuzingatia
matakwa ya kifungu cha 44(5) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za
Mitaa, Sura ya 292, kikisomwa pamoja na Kanuni ya 28(1)(2) ya Kanuni za
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Uchaguzi wa Madiwani) za mwaka 2015.
“Tume,
ilipokea, ilijadili na kufanya maamuzi ya Rufaa 25 ambapo jumla ya
wagombea kumi (10) walifanikiwa na hivyo kuendelea na uchaguzi na
wagombea 15 rufaa zao hazikufanikiwa na hivyo kutoendelea kuwa
wagombea,” amesema Dkt. Kihamia.
Ameongeza
kuwa katika kata sabini na saba (77) wanachama 254 kutoka vyama kumi na
moja (11) vya siasa walichukua fomu za uteuzi na kwamba jumla ya
wanachama 186 sawa na asilimia 73.2 ya waliochukua fomu za uteuzi
walizirejesha na kuteuliwa kuwa wagombea ambapo kati yao wagombea 179
sawa na asilimia 96.2 ni wanaume na wagombea 7 sawa na asilimia 3.8 ni
wanawake.
“Hadi
muda wa mwisho wa uteuzi ulipofika (saa 10.00 jioni siku ya uteuzi)
wanachama 68 sawa na asilimia 26.8 ya waliochukua fomu hawakuteuliwa
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kutorudisha fomu, kurudisha fomu
nje ya muda unaokubalika kisheria na fomu kutojazwa ipasavyo,” amesema.
Dkt.
Kihamia amefafanua kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa madiwani
utakaofanyika Agosti 12 mwaka huu jumla ya vyama kumi na moja (11)
vimesimamisha wagombea.
Amewataja
Wagombea hao katika Kata kwa kila Chama kuwa ni ACT-Wazalendo Wagombea
17 (sawa na asilimia 22), ADC Wagombea 3 (sawa na asilimia 3.9), CCM
Wagombea 77 (sawa na asilimia 100) CHADEMA Wagombea 54 (sawa na asilimia
70), CHAUMMA Wagombea 2 (sawa na asilimia 2.6), CUF Wagombea 17 (sawa
na asilimia 22), Demokrasia Makini Wagombea 4 (sawa na asilimia 5.2),
NCCR-MAGEUZI Wagombea 6 (sawa na asilimia 8), NRA Wagombea 3 (sawa na
asilimia 3.9), SAU Mgombea 1 (sawa na asilimia 1) na UPDP Wagombea 2
(sawa na asilimia 2.6).
Wakati
huohuo, Dkt. Kihamia amesema kwamba katika jimbo la Buyungu jumla ya
wanachama kumi (10) kutoka vyama kumi (10) vya siasa vya AAFP,
ACT-Wazalendo, CCM, CHADEMA, CUF, DP, Demokrasia Makini, NRA, UMD na
UPDP walichukua fomu za uteuzi.
“Wanachama
wote kutoka vyama hivyo walirejesha fomu na kuteuliwa kuwa wagombea wa
Ubunge katika Jimbo hilo, kati yao wanaume ni tisa (9) na mwanamke mmoja
(1),” amesema Dkt. Kihamia.
Amevitaka
vyama vya siasa na wagombea wao kuzingatia maadili ya uchaguzi wa Rais,
Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2015, wakati wote wa kampeni na siku ya
uchaguzi.
Mpekuzi.
Comments