Mbunge
wa Jimbo la Mtama, Mh. Nape Nnauye amesema kwamba wanaomzushia kwamba
amesimamiswa uanachama wa Chama Cha Mapinzduzi watapata tabu sana.
Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba barua ya Mbunge huyo kusimamishwa uanachama wa Chama chake imekwishamfikia mkononi.
"Kwa
uzushi huu watapata tabu sana wanuka maziwa, ndio shida ya kudandia
treni kwa mbele, unawakuta wenyeji unakuwa Mwenyezi kuliko" Nape Nnauye.
Mwenyekiti
wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi John Pombe Magufulia mapema wiki hii
alionyeshwa kuchukizwa na wabunge wanaotokea mikoa ya Lindi na Mtwara
kutokana na michango yao bungeni kwenye suala la korosho ambapo baadhi
ya wabunge wa CCM kutokea mikoa hiyo waliitaka serikali iwalipe wakulima
pesa ambazo wanadai ili waweze kuendeleza zao hilo.
Hivi
karibuni Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado
Shaibu alidai kwamba hakuna mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa
akiwa chini ya Chama tawala hivyo kuwahimiza Nape, Bashe na Hawa Ghasia
kuwa kama wana nia ya dhati ya kuwatetea wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.
Mpekuzi.
Comments