Mwanafunzi atoroka kambi akimbilia kwa mwanamme.

KATIKA hali isiyo ya kawaida mwanafunzi anayesoma kidato cha nne skuli ya sekondari Makunduchi (jina limehifadhiwa), ameondoka kwenye kambi ya kujiandaa na mitihani ya taifa na kwenda Jambiani kwa anayeaiwa kuwa mpenzi wake.
Mwanafunzi huyo pamoja na wenziwe walitolewa kwa muda kambini ili kupata fursa ya kusherekea sherehe za kijadi zinazofanyika kila mwaka kijini hapo za mwaka kogwa, ambapo alitumia fursa hiyo kwenda Jambiani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, msaidizi mwalimu mkuu wa skuli hiyo Zimba Khatib, alisema siku ya sherehe za mwaka kogwa wanafunzi wote walitolewa majira ya saa 5 asubuhi hadi saa 8, ili kujumuika kwenye sherehe hizo.
Mwalim Zimba alisema katika hali ya kusikitisha mwanafunzi huyo hakurejea kwenye kambini ya kujinadaa na mitihani ya taifa katika muda uliopangwa.
Alisema kikawaida katika kambi hiyo wanafunzi wanaojiandaa na mitihani ya taifa hawawaruhusu kutoka isipokuwa kwa dharura maalumu kama hiyo ma kupata ruhusa ya wazee wake.
Hata hivyo, alisema baada ya kumfuatilia kwa wazee wake waligundua kuwa hata nyumbani kwao hakuwepo kwa siku hiyo ambapo alirudi nyumbani kwao siku ya pili.
Babu wa mwanafunzi huyo akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa baada ya kumuhoji mjukuu wake alikiri kuwa alikwenda kwa mwanamme huyo mkaazi wa Jambiani.
Zanzibarleo.

Comments