Omar al-Kiswani, mkuu wa msikiti huo amesema kuwa, kuporomoka kwa mawe ya eneo la makumbusho ya Kiislamu karibu na eneo la Babul-Magharibah na ukuta wa Buraq upande wa magharibi wa msikiti wa al-Aqsa, kumetokana na mashimo yanayoendelea kuchimbwa na utawala haramu wa
Kizayuni katika eneo hilo la makumbusho ya Kiislamu. Kadhalika al-Kiswani amesema kuwa, utawala wa Kizayuni umezuia kuingia wataalamu na wahandisi wa kitengo cha waqfu za Kiislamu katika eneo la magharibi mwa msikiti huo kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kufuatilia suala hilo.
Kadhalika amesema kuwa, kuporomoka mawe ya ukuta huo kumeongeza shaka na wasi wasi juu ya mashimo yanayochimbwa na utawala huo khabithi katika eneo tajwa.
Hivi karibuni pia, Izam Khatwib, mkuu wa idara ya waqfu wa Kiislamu na masuala ya msikiti wa al-Aqsa alitahadharisha juu ya mashimo ya utawala wa Kizayuni katika eneo la makumbusho ya Kislamu magharibi mwa msikiti huo.
Utawala wa Kizayuni unaendelea kuchimba mashimo chini ya msikiti wa al-Aqsa kwa lengo la kuanzisha hekalu bandia la Kiyahudi mahala pa msikiti huo.
Comments