Alisema sio sahihi serikali inawabeza wakulima wa mwani, kama inavyoelezwa na baadhi ya kampuni zinazonunua zao hilo, kwa kusema hakuna hata sera inayowalinda wakulima hao.
Alisema hayo kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya mwani Zanzibar, hafla iliofanyika kijiji cha Mfikiwa wilaya ya Chake Chake, zilioandaliwa na Milele Foundation na wadau wake.
Alisema, kama zipo kampuni za mwani zinafikiria kuwa, serikali haina habari na wakulima wa mwani, wabakie na dhana zao hizo, lakini pia waendelea na kuwa mashahidi jinsi serikali inavyobuni mbinu za kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanaishi maisha ya raha.
Aliyataja mikakati hayo kuwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kusarifia mwani ambapo kwa sasa watafiti wa ndani wanaendelea na kufanya utafiti ili kujua wapi kiwanda hicho kijengwe.
Aidha alisema serikali imewahi kutoa vihori 500 kwa wakulima Unguja na Pemba kwa ajili ya kufanikisha kazi za kilimo hicho.
Zanzibarleo.
Comments