Katibu Mkuu CCM Awamwagia Sifa Kibao Nape Nnauye na Hussein Bashe......Awapeleka Kuzindua Kampeni Jimbo la Buyungi.
Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally amesema wabunge
wawili miongoni mwa saba watakaoongoza kampeni za ubunge wa chama hicho
kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu ni watukutu na wadadisi, ambao
CCM inapaswa kujivunia.
Aliwataja
wabunge hao kuwa ni Hussein Bashe (Nzega) na Nape Nnauye (Mtama), ambao
kwa sasa CCM inapaswa kujivunia kutokana na namna wanavyodadisi mambo
na kuyafuatilia, jambo linalofanya mawaziri wafikiri kwa kina kabla ya
kutoa majibu na maamuzi.
Dk.
Bashiru aliyasema hayo Jumanne ya wiki hii alipokuwa akizungumza na
wanachama wa CCM alipopita wilayani Nzega wakati akielekea Kigoma kwenye
kampeni za uchaguzi huo zilizozinduliwa jana.
Alisema
anamshukuru Bashe kwa kukubali kuwa miongoni mwa wabunge saba
watakaoshiriki uzinduzi kampeni hizo katika Jimbo la Buyungu.
Wabunge
wengine watakaoshiriki kwenye kampeni hizo ni Job Lusinde (Mtera),
Martha Mlata (Viti Maalumu CCM), Munde Tambwe (Viti Maalumu CCM), Sixtus
Mapunda (Mbinga Mjini), Jackline Ngonyani (Viti Maalum CCM).
“Na
kupitia kwenu ningependa kufafanua kuwa Hussein Bashe si mwanachama
mkorofi katika chama, lakini ni miongoni mwa wabunge wadadisi, maana
kuna tofauti kati ya ukorofi na udadisi na kwa udadisi wake anasababisha
tetesi zisizokuwa na ukweli.
“Niwahakikishie,
namfahamu kabla hajawa mbunge, Bashe ni mtu mdadisi katika maisha yake
niliyomjua mie, ana tofauti kidogo na Nape, Nape kidogo ana joto zaidi
kuliko Bashe lakini wote mimi ninawafahamu ni wanachama wadadisi kwa
hulka zao.
“Nawafahamu
kuwa ni watukutu kweli kweli, wadadisi kwelikweli, lakini wanapishana,
kwa kuwa Nape ni mdadisi na mtukutu ambaye joto lake ni kali hivyo kazi
yake ni kupooza,” alisema.
Alisema
kutokana na udadisi wao na kile ambacho watu wengine wanaona kama ni
utukutu, ilifikia wakati baadhi ya wanachama na watu ndani ya CCM
walianza kutaka waondolewe, suala ambalo yeye hakubaliani nalo.
Alisema
Nape na Bashe ni mfano mzuri wa wabunge wanaochochea usimamizi na
kuibua mijadala mizito yenye manufaa kwa Bunge, chama na Serikali.
Dk.
Bashiru alisema wanapoona joto linazidi kazi yao ni kulipunguza, kwa
kuwa wanapozungumzia nidhamu hawazungumzii kunyamazisha watu kwa sababu
kufanya hivyo kutafanya kukosekane mijadala na fikra mpya.
“Kwa
hiyo msikubali kudanganywa kwamba Bashe na Nape ni watukutu, si
watukutu, ni wadadisi kwa hiyo ninawashukuru sana kumchagua Bashe maana
anachangamsha Bunge na anawafanya mawaziri wa CCM kufikiri kabla ya
kutenda.
“Maana
kutenda kila mmoja anaweza kutenda, hata mwendawazimu anaweza kutenda
lakini ili utende kwa ufanisi na tija unahitaji kufikiri na kwa hiyi
michango yake katika Bunge inawafanya mawaziri wafikiri,” alisema.
Alisema
mahudhurio ya Bashe na Nape bungeni ni mazuri na kuwapa alama ya A na
kwamba amepitia mahudhurio na kuona wapo wabunge wasiohudhuria bungeni
na wengine hawajawahi kuwasikia hata mara moja wakichangia.
Alisema
ameanza kuchambua mahudhurio hayo tangu kuanza kwa Bunge hadi siku ya
bajeti na kubaini kuwa baadhi ya wabunge walihudhuria kikao kimoja tu
kati ya 15 vya wabunge wa CCM (part caucus).
“Tena waliingia katika vikao vilivyokuwa vinahusu agenda inayowahusu,” alisema.
Alisema
watatumia kanuni kuwaadabisha hadi watakaposhika adabu na kuwataka
wabunge watambue kwamba ubunge ni mali ya wananchi kupitia chama
kilichowadhamini.
Dk.
Bashiru alisema kwa kuwa hakuna utaratibu wa wapiga kura kuwawajibisha
wabunge kabla ya muda, watashughulikiwa ndani ya chama.
Alisema
shabaha ya tatu ya Ilani ya CCM ni kupambana na rushwa na ufisadi bila
woga kwa rais aliye madarakani na katibu mkuu wa chama kutokuwa wala
rushwa ili mashambulizi yaanzie Ikulu na makao makuu ya chama.
Mpekuzi.
Comments