Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe .Profesa Ibrahim Juma amewataka mahakimu wapya wasiwe chanzo cha ucheleweshaji wa mashauri.
Aidha
kuacha kulalamika bali pale linapotokea matatizo, bali wawe chachu ya
kuyatafutia ufumbuzi katika utendaji wao wa kazi wa kutoa huduma za
haki kwa wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Jaji Mkuu huyo wakati akiwaapisha Mahakimu
wapya kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama Kuu jijini
Dar es Salaam.
“
Kiapo mlichoapa ni uzito muda wote mtakaofanya kazi ya kuwatumikia
wananchi, wananchi wanataka kutatuliwa kwa malalamiko yao kwa haraka,”
Aliongeza
kwamba mfumo wa sasa sio wa kukaa na kulalamika, kama kuna tatizo
litafutiwe ufumbuzi na kuepuka kuwa chanzo cha ulalamishi.
Alisema
mahakimu hao wanapaswa kuwa weledi wanapotoa huduma za utoaji haki
ili waweze kutoa hukumu zinazoeleweka kwa kujibu wa sheria na kanuni.
Hivyo wanapaswa kushirikiana na wadau wengine wa mahakama ili
kuahakikisha hukumu zinatoka kwa haraka.
Alisisitiza mahakimu hao kwamba kufanya kazi kwa kuepuka rushwa na kwa nidhamu.
Jaji
Mkuu huyo alifafanua kuwa changamoto za majengo chakavu na umbali ,
visikwamishe utendaji kazi wao, hivyo mahakama iko katika Mpango
Mkakati wa Miaka Mitano ambao unalenga kutoa huduma za haki kwa
wote na wakati, ikiwemo kuboresha miundombinu.
Aliwataka mahakimu hao kuielewa taasisi inayofanyakazi na mpango mkakati huo.
Mpekuzi.
Comments