Naibu
Waziri wa Áfya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt
Faustine Ndugulile amegoma kuzindua Majengo ya chuo chá Áfya chá Waganga
Wasaidizi Mkoani Mara kutokana na kutoridhishwa na Matumizi ya fedha ya
kiasi cha shilingi Milion 500 kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa Majengo katika Chuo hicho.
Hayo
yamejiri mapema jana wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua shughuli
za ujenzi na ukarabati wa Majengo ya chuo hicho kilichopo Musoma, ikiwa
ni mwendelezo wa ziara yake katika kukagua hali ya utoaji huduma za
afya Mkoani hapo.
“Nimekuja
hapa, kazi ya milioni 500 sijaiona kabisa ,kilichofanyika mmepiga
rangi, kuta mbovu na Siwezi kuwa katika dhambi ya kuhararisha, kwahiyo
nimegoma uzinduzi wa Majengo haya, na nimeagiza kwa chuo kupata maelezo
kwa wote walishiriki na kuahidi kuwachulia hatua wote walishiriki ”
alisema Dkt. Ndugulile
Dkt.
Ndugulile alitoa onyo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Juu ya fedha
nyingine zilizopelekwa kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa vituo Saba
vya utoaji wa huduma za Afya katika mkoa wa Mara na kumtaka kusimamia
kikamilifu matumizi ya fedha z vituo hivo ili viweze kuwasaidia wananchi
wa Mara.
“Tumeleta
tena fedha zingine kwaajili ya ujenzi wa vituo vya Áfya saba, naomba
hizo fedha za umma tukazisimamie vizuri kwa ukamilifu, kama ukaona
wenzako hawaendi katika njia sahihi, toa taarifa ili ujiokoe wewe, na
wewe ukiwa katika sehemu ya kuhararisha ile dhambi dhoruba hii na wewe
itakukumba ” alisema Dkt.Ndugulile.
Pia
Dkt. Ndugulile alitembelea kituo chá Áfya chá Bunda ambacho
kinatambulika kama Hospitali ya Wilaya Dkt. Ndugulile aliagiza
kusimamishwa kazi kwa Mganga Mkuu wa Mji wa Tarime kutokana na uzembe wa
usimamizi mbovu wa huduma za afya katika kituo hicho, huku akimtaka
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Lydia Bupilipili kuhakikisha anasimamia agizo
hilo.
“Mambo
haya yote yanatokea kwasababu ya usimamizi mbovu Kwaiyo nimeagiza
Mganga Mkuu wa Mji (TMO) asionekane hapa, kamati ya mkoa wamchukue
aletwe mtu mwingine anaeweza kusimamia, huyu mtu hatufai akapangiwe
majukumu mengine, na Mkimruhusu tutaanza kuwajibishana sisi, tunataka
kuijenga Bunda mpya ” alisema Dkt. Ndugulile.
Vilevile
Dkt. Ndugulile alimwagiza Mganga mkuu wa mkoa wa kupitia upya Matumizi
matumizi ya jengo jipya lililojengwa kwaajili ya kuhifadhi maiti Kwani
haliendani na mahitaji kutokana na ukubwa wake, hivyo kuagiza
kubadilisha matumizi ya jengo hilo na kulifanya kuwa jengo la x-ray.
“nimetembelea
jengo la mochwali, jengo ni kubwa kuliko hata jengo la mochwali lá
Muhimbili, sambamba na hilo nimeambiwa Kwamba kuna vifaa vya x-ray
vimeletwa, Sasa nimetoa maelekezo Kwamba tubadilishe matumizi, lile
jengo tunaweza kutumia kwa huduma za jengo la x-ray, nitaagiza wataalamu
wangu waje kupitia jengo hilo ili tufunge vifaa vya x-ray, kazi ianze ”
alisema Dkt Ndugulile.
Mpekuzi.
Comments