Dk. Shein apongeza utendaji ofisi ya Rais.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, ameupongeza uongozi na wafanyakazi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa utendaji mzuri.

Dk. Shein  aliyasema hayo, ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati ulipowasilisha utekelezaji wa mpango kazi wa mwaka 2017/2018 na mpango kazi wa utekelezaji kwa mwaka 2018/2019.

Huo ulikuwa mkutano wa mwisho kwa kipindi hichi kwa utaratibu aliojiwekea Dk. Shen wakukuna na viongozi na watendaji wa wizara mbalimbali.

Alitoa pongezi za dhati kwa uongozi na wafanyakazi wa ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa utendaji mzuri wa kazi zao, hatua inayompelekea kuendelea kufanyakazi vyema za kuwatumikia wananchi.

Alieleza kuwa uwasilishwaji mzuri wa mpango kazi wa Ofisi hiyo umetokana na uzoefu wa muda mrefu uliopatikana tangu kuanza kwa zoezi hilo la bango kitita ambalo lilianza mara tu alipoingia madarakani.

Dk. Shein alimpongeza waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi kwa kumsaidia katika shughuli mbali mbali za kazi na kumpongeza Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee kwa utendaji wake mzuri.

Aidha, aliwashukuru na kuwapongeza washauri wake wote kwa kuendelea kumshauri mambo mbalimbali ya msingi na kutoa nasaha kwa uongozi wa ofisi hiyo huku akiwataka kuwasikiliza.

“Nimeshuhudia uwezo mkubwa mlionao wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na nimethibitisha hili kwa kufuata ule msemo usemao  ukitaka kuwajua wafanya kazi wa ikulu wape kazi”,alisema.

Zanzibarleo.

Comments