Dk. Khalid mageuzi ya kiuchumi yameleta mafanikio.

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed amesema, Zanzibar ipo katika mageuzi makubwa ya kiuchumi huku mafanikio yakionekanwa chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohamed Shein.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa mali za serikali, huko katika ukumbi wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu na Mthibiti wa Fedha za Serikali Mazizini Mjini Unguja.

Alisema kumekuwa kumekuwepo mageuzi makubwa yakiwemo ya kiuchumi ikiwa na lengo la kupeleka maendeleo katika jamii.

Alisema kwa sasa hali imekuwa ikionekana hasa katika sekta ya afya, elimu, miundombinu ikiwemo ujenzi wa majengo mapya ya kisasa.

Akizungumzia katika sekta ya afya, Dk. Khalid alisema serikali imeweza kuimarisha huduma za afya kwa wananchi wake na madaktari wake wamekuwa akipatiwa mafunzo sambamba na kupelekwa vifaa mbalimbali katika vituo vya afya.

Mbali na hayo alisema hivi karibuni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein alitangaza kwa hospitali za serikali, dawa na vifaa tiba vyote vitaharamia na serikali na vitolewe bure.

Zanzibarleo.

Comments