Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai sababu kubwa ya kuondoka
aliyekuwa Mbunge wa Ukonga na mwanachama wa chama hicho, Mwita Waitara
ni kutokana na hofu ya kukosa Ubunge mwaka 2020 kutoka na safu yake ya
viongozi kushindwa kupata nafasi.
Hayo
yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje
wa Chadema, John Mrema ikiwa imepita siku moja tokea Mbunge huyo
kutangaza hadharani kujivua uanachama wake na kujiunga na Chama Cha
Mapinduzi (CCM), huku kudai sababu kubwa ya yeye kuchukua maamuzi hayo
ni kutokana na ugomvi wake na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani
ya chama.
Sababu
nyingine za Mwita Waitara kuondoka CHADEMA amedai kwamba ndani ya chama
hicho hakuna ruhusa ya Mbunge kusema lolote, hakuna uchaguzi wa haki
bali kuna pachika pachika pamoja na Mbowe kutotaka kushauriwa.
"Anaposema
hakuna uchaguzi ndani ya chama ni muongo, jimbo la Ukonga tulifanya
uchaguzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya misingi, tukaenda matawi, kata
na hatimaye Wilaya. Mwita alikuwa amepanga safu yake ya viongozi ambayo
imeshindwa na kulalamika sana kwanini safu yake ilishindwa..
"Walishindwa
kutokana na wapiga kura waliamua kuchagua viongozi wengine na hicho
ndicho kilimfaya Mwita kuwa na hofu ya kukosa Ubunge katika chaguzi
zijazo na amelalamika kwa maandishi", amesema Mrema.
Mbali
na hilo, Mrema amemtaka Mwita Waitara kutoa sababu za msingi za
kuondoka ndani ya chama hicho nasio kufanya siasa nyepesi za kuchafuana.
Mwita
Waitara amekuwa Mbunge wa pili kutoka CHADEMA kujivua Ubunge, ambapo
Mbunge wa kwanza alikuwa Dkt. Godwin Oloyce Mollel mnamo Disemba 14,
2017 alitangaza kujivua rasmi uanachama wa chama hicho na kujiunga na
CCM kwa madai ya kuunga mkono utendaji ya Rais Magufuli.
Mpekuzi.
Comments