Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema hatamwonea aibu
kiongozi au mtu yeyote atakayetaka kuhatarisha amani ya nchi.
Kutokana na hali hiyo, amesema kuanzia sasa, wanaotaka kuhatarisha amani, wajue kwa sasa ameuvaa uninja usoni.
Waziri
Kangi aliyasema hayo jana mjini hapa alipokuwa akizungumza na viongozi
wa taasisi, mashirika, mamlaka na taasisi za Serikali pamoja na wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkoa wa Mbeya.
Katika
maelezo yake, waziri huyo aliwataka viongozi wajiandae kwa uamuzi mgumu
atakaoutoa baada ya kupokea taarifa kutoka kwenye mamalaka husika
zinazojihusisha na usalama barabarani.
“Nilipokuwa
bungeni, kuna baadhi ya watu walionekana kutaka kuharibu amani na mimi
kulazimika kuvaa kofia ya kininja ambayo ilikuwa ya kitambaa.
“Lakini, kwa sasa nitalazimika kuvaa kofia hiyo ya chuma na nzito zaidi kwani ninaopambana nao ni makamanda wenzangu.
“Niliapishwa
Jumatatu wiki hii kushika nafasi hii inayoyahusisha majeshi ya
magereza, uokoaji, idara ya uhamiaji, vitambulisho vya Taifa,
wakimbizi, usajili wa vyama vya kijamii, makanisa na misikiti.
“Kwa kawaida, vyombo vyote hivyo ndivyo vinavyohakikisha amani ya nchi inakuwepo.
“Hivyo
basi, wananchi wanapopata ajali mahali popote ikiwamo Mbeya na maeneo
mengine ya nchi na wakati huo huo Serikali ikashindwa kuchukua hatua,
basi nchi haitakuwa na amani wala utulivu.
“Kwa hiyo, sitanii bali nimeamua kuuvaa uninja nikimaanisha na sitamwonea haya mtu yeyote."
Mpekuzi.
Comments