10 mbaroni kwa kukutwa na nyara za Taifa.

Polisi wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wanawashikiria watu kumi kwa kosa la kukutwa na nyara za Taifa kinyume cha sheria.

Kamanda wa Polisi mkoa huo, Juma Ndaki akizungumza na waandishi jana  Jumapili Julai 22, 2018 alisema watuhumiwa hao wamekutwa na vipande 531 vya nyama kavu, mikia 24 ya nyumbu, mikia 12 ya pundamilia, nyaya 75 za kutegea, mapanga mawili,  visu viwili, dumu nane za maji na baiskeli 10.

Ndaki alisema mzigo huo ulilkamatwa kwenye kambi yao ya ujangili eneo la  Togoro ndani ya Hifadhi ya Taifa ya  Serengeti kwa ushirikiano wa  askari wa  Hifadhi hiyo na  Polisi wilayani humo.

“Watuhumiwa wote ni wakazi wa kata za Nyambureti na Nyamatare wilayani Serengeti,” alisema Ndaki
Mpekuzi.

Comments