Watendaji wa Wizara ya Afya Pemba waanza kutekeleza agizo la Waziri.


Image result for hamad rashid mohamed
Uongozi wa wizara ya afya kisiwani pemba umeanza utekelezaji wa agizo la ,waziri wa afya zanzibar mh hamad rashid muhammd,  la uwekaji wa vikuta na alama kwa hospitali ya vitongoji  kwenye maeneo ya nje ya jengo hilo ili kuepuka uharibifu unaofanywa na wanajamii kwa ufungaji wa mifugo yao.

Agizo hilo alilitoa wakati alopofanya ziara hospitalini hapo mara tu baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kuona haridhishwi na hali aloikuta  juu ya uharibifu unaofanywa na wafugaji kwa kulitumia eneo hilo la wazi kama sehemu malishio ya manyama wao.

Kauli hiyo imetolewa na afisa mipango wa idara ya mipango sera na utafiti wa wizara ya afya pemba ali suleiman othman , wakati alipofika hospitalini hapo kuonana uongozi wa hospiali ya vitongoji na kukagua maeneo mbali mbali ili kuweza kujua changamoto zinazo wakabili watendaji wa hapo.

Amefahamisha kwamba umoja mashirikiano kazini kutawezesha kusimamia majukumu ya kazi na  kuyatekeleza pamoja na kuweka sawa maeneo ya jengo la hospitali ili kuona uharibifu hautokei.

Aidha amefahamisha kwamba eneo la nje ya jengo hilo wamefika kueka alama za vibati na vikuta kuonyesha kwamba ni marufuku kutumiwa na wananchi hasa kwa wanaofuga ngombehulitumia  na kupelekea uharibifu na uchafuzi wa mazingira.

Nae afisa ufatiliaji na tathmini wa idara ya mipango sera na utafiti kutoka wizara ya afya pemba abdalla muhamed ali, amemuomba dakar dhamana kumsimamia kila mtendaji ambae amepewa dhamana ya ushughulikiaji wa kitu na utoaji huduma ili kuona kasoro ndogo ndogo zinaondoka hospitalini hapo.

Hata hivyo amemuhimiza juu ya usafi na utunzaji wa vifaa vya hospitali ili kuona vinadumu na kutoa huduma.

Aidha amemuomba kuvitunza vitu chakavu na kuweka sehemu moja na kuvitambua vinavyofanya kazi na visivyofanya kazi ili kutambuliwa na kufanyiwa hatua nyengine za kiutendaji.

Daktar dhamana hospitali ya vitongoji najma said khelef, amesema mashirikiano kazini yapo kwa watendaji wake kwani amekua akisikiliza kero zao na kuzitatua.

Kuhusu usafishaji waeneo la nje alisema vijana wa uvccm walipanga kuenda kufanya usafi ikiwa ni mchango wao katika kuhamasisha huduma na uwekaji safi wa mazingira.

Comments