Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. Shukrani Manya leo tarehe 28 Juni,
2018, amepokea ripoti ya Ukaguzi Maalum wa Migodi ya Madini ya Vito na
Madini ya Kinywe (Graphite) kutoka kwa Mwenyekiti wa Timu ya Ukaguzi
Profesa Justinian Ikingura.
Ripoti
hiyo imetokana na Tume Maalum ya Wataalam Sita iliyoundwa na Katibu
Mtendaji wa Tume ya Madini Prof. Manya tarehe 17 Juni, 2018 ikilenga
kufanya ukaguzi maalum katika maeneo ya uchimbaji wa madini ya Vito na
Kinywe katika wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro.
Aidha,
ukaguzi huo ulilenga kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Madini
Doto Biteko aliyoyatoa hivi karibuni wakati wa ziara yake mkoani
Morogoro.
Katika
ziara ya Naibu Waziri Biteko mkoani humo, alipokea malalamiko kutoka
kwa wachimbaji wadogo wa madini ya vito ambao ni wanakijiji wa kijiji
cha Epanko kilichopo katika eneo la mradi wa madini hayo.
Aidha,
kufuatia malalamiko hayo Naibu Waziri aliahidi kuunda timu ya watalaam
wa madini itakayofanya kazi ya ukaguzi maalum kwa lengo la kutathmin
uendeshwaji wa migodi ya madini ya vito na kinywe pamoja na biashara ya
madini kulingana na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 pamoja na marekebisho
yake.
Katika
ripoti hiyo, timu ya wataalam wa madini imetoa mapendekezo mbalimbali
ikiwemo Serikali kupitia Wizara ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na
Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuweka mkakati wa kufanya Utafiti na
tathmin ya madini adimu ya vito katika eneo la Mahenge na maeneo mengine
nchini ili kuwepo na takwimu sahihi za kuvutia wawekezaji katika
uchimbaji wa madini hayo.
Pendekezo
lingine ni Mamlaka husika kuweka mpango wa kutoa huduma ya
uthaminishaji wa madini ya vito katika maeneo ya wachimbaji wadogo ili
kuwezesha wachimbaji hao kupata bei stahiki ya madini wanayozalisha na
hivyo kuongeza kipato chao na kulipa tozo stahiki kwa Serikali.
Wajumbe
wa timu hiyo walitoka katika Taasisi ya Jiolojia ya Utafiti wa Madini
Tanzania (GST), Chuo cha Madini Dodoma, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Kamishna Msaidizi Ukaguzi wa Migodi na Afisa Madini Mkazi wa Dodoma.
Mpekuzi.
Comments