Rais wa Zimbabwe: Siku yangu ya kufa bado haijafika.

Rais wa Zimbabwe: Siku yangu ya kufa bado haijafikaRais wa Zimbabwe amesema baada ya kunusurika kifo katika mlipuko wa jana kwamba, siku yake ya kufa ilikuwa haijafika.

Rais Emmerson Mnangagwa amesema hayo muda mfupi tu baada ya kunusurika kifo kufuatia mlipuko uliotokea katika mkutano aliokuwa anauhudhuria mjini Bulawayo. 
Rais huyo wa Zimbabwe amesema kuwa, alikusa masafa mafuupi mno kutoka sehemu ulipotokea mlipuko huo.
Video kutoka uwanja wa michezo wa White City inaonesha Rais Mnangagwa akiondoka kwenye jukwaa baada ya kutoa hotuba, mlipuko unapotokea. 
Msemaji wake amesema rais huyo alinusurika na kwamba, hakupata majeraha yoyote.
Msemaji wa rais George Charamba ametoa taarifa akisema: "Kumekuwa na majaribio kadha ya kumuua rais miaka mitano iliyopita."
Gazeti la serikali la Herald limeripoti kuwa Makamu wa Rais Kembo Mohadi ameumia miguuni wakati wa mlipuko huo unaodhaniwa kutokana na bomu, lakini taarifa hizo hazijathibitishwa.
Maafisa wengine kadhaa wakuu serikali pamoja na walinzi wamejeruhiwa katika tukio hilo la mripuko wa bomu ambalo lilizua taharuki kuubwa.
Tukio hilo limekwenda sambamba na mlipuko mkubwa bomu uliotokea jana katika mkutano wa Waziri Mkuu mpya wa Ethiopia, Abiy Ahmed. 
Inaarifiwa kwamba watu 83 wamejeruhiwa huku 6 wakiwa katika hali mahututi. 
Ilibidi kiongozi Waziri Mkuu huyo aondoshwe haraka muda mfupi baada ya kutoa hotuba yake wakati mlipuko huo unaodhaniwa kuwa wa guruneti, ulipotokea. 
Maelfu walikuwa wamekusanyika katika bustani kuu ya Meskel mjini Addis Ababa katika mkutano ulioandaliwa kuiunga mkono serikali yake Abiy.
parstoday.

Comments