Alitoa kauli hiyo uwanja wa ndege wa Abeid Aman Karume, wakati akikabidhiwa mwenge wa uhuru kutoka Mkoa wa Lindi na Mkuu wa Mkoa huo, Godfrey Zambi, ambao tayari umeanza mbio zake ndani ya mkoa huo.
Alisema serikali inajitahidi kupiga vita udhalilishaji, lakini inaonekana vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka.
Alisema kupitia mwenge huo, anaimani vitendo vya udhalilishaji vinaweza kupungua kwa kiasin kikubwa.
Mkoa wa Kusini unaongozwa kwa vitendo vya udhalilishaji Zanzibar.
Pia alisema qatahakikisha wanapiga vita ukimwi, rushwa, malaria na matumizi ya dawa za kulevya.
Hivyo aliwaomba wananchi kuupokea mwenge wa uhuru kwa moyo mkunjufu, ili uweze kuwaletea tija na maendeleo ndani ya mkoa wao.
Akikabidhi mwenge huo, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, alisema katika mkoa wake mwenge walifanikiwa kuzindua miradi 41 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.
Zanzibarleo.
Comments