
Tukio hilo linalohusishwa na wivu wa kimapenzi, limetokea baada ya Zaid kumtuhumu mke wake kukosa uaminifu ndani ya ndoa, hali iliyomlazimu kufanya jaribio la kutaka kumchoma kwa kisu, ambalo halikufanikiwa kabla ya kuamua kuchoma moto nguo hizo.
Taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa Habari na Ofisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani Hassani Mtengefu, ikisainiwa na Kamanda ACP Jonathan Shanna, imeeleza kuwa tukio hilo limetokea nyumbani kwao Mtaa wa Kilimahewa mjini hapa.
Imefafanua kwamba Juni 25 eneo la kwa mama Rose Kata ya Mailimoja, mkazi huyo mfanyabiashara baada ya kutokea hali ya sintofahamu hiyo, alichukua kisu kwa lengo la kutaka kumshambulia mwilini, baada ya kumkosa akaamua kukusanya nguo zote kisha kuziwasha kwa kutumia kiberiti.
Imeongeza kuwa baada moto kushika kasi, wananchi walifika wakisaidiana na Polisi wakafanikiwa kuwaokoa watu hao, hatimae kuwakimbiza Hospitali Teule ya Tumbi kwa ajili ya matibabu.
Juhudi za madaktari hospitali ya Tumbi ziliposhindikana wakawakimbiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi ambapo hata awakuweza kuokoa uhi wa watu ho ambapo mwanamme amefariki Juni 25, mwanammke Juni 26.
Zanzibar24.
Comments