Alisema hayo huko Uroa katika ufunguzi wa mradi huo ambapo
alifahamisha kwamba thamani ya mradi huo ni kubwa na hailingani na
thamani ya ujenzi wa mradi na kwamba hatokifungua kituo hicho.
Mradi wa kituo cha afya Uroa wenye chumba cha kutolea huduma za mama
wajawazito na watoto, chumba cha ushauri nasaha, maabara na huduma
nyengine umegharimu shilingi milioni 382 hadi kumalizika kwake.
Akitoa salamu za mbio za mwenge wa uhuru kwa wananchi mbalimbali
kiongozi huyo amesisitiza umuhimu wa wazazi kuwekeza katika elimu kwa
maendeleo ya taifa na watoto wao.
Alifahamisha kwamba serikali zote mbili ya Zanzibar na Tanzania bara
zinaendelea na jitihada zake za kuimarisha sekta ya elimu kuanzia ngazi
ya msingi hadi chuo kikuu.
Zanzibarleo.
Comments