Michuano
ya mwaka huu ya Kombe la Kagame inachezwa nchini baada ya mara ya
mwisho kufanyika nchini pia mwaka 2015 ambapo Azam FC ilitwaa ubingwa
kwa kuifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0.
Katibu
Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA),
ambao ndiyo waandaaji wa Kombe la Kagame, Nicolas Musonye amesema mpaka
sasa wamejiandaa vizuri kufanikisha michuano hiyo.
“Kila
kitu kipo sawa na leo michuano hii tutaifungua rasmi na naamini
tutafanya michuano bora na yenye wachezaji bora wanaoweza kupambana,”
alisema Musonye.
Musonye aliishukuru Azam TV kwa udhamini wake ikiwemo kuonyesha moja kwa moja mechi za Kombe la Kagame mwaka huu.
Mkurugenzi
wa Michezo wa Azam Media, Patrick Kahemele alisema wao wamejipanga
vizuri kufanikisha michuano ya Kombe la Kagame ambayo itaanza leo kwenye
viwanja viwili vya Azam Complex na Taifa.
Kaimu
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani
alisema wao kama TFF wamejiandaa ipasavyo kukamilisha michuano hiyo ya
Kombe la Kagame.
Leo
katika ufunguzi mechi za Kundi A ndizo zitakazokuwa za kwanza kuchezwa
ambapo JKU ya Zanzibar itapambana na Vipers ya Uganda saa 8:00 mchana
halafu itafuatiwa na mchezo wa Azam FC na Kator ya Sudan Kusini.
Saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa, utachezwa mchezo wa Kundi C kati ya Singida United na APR ya Rwanda.
Zanzibarleo.
Comments