Staa
wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amemwaga povu zito kwa
mashabiki waliokuwa wanamnanga mtoto wake aliyezaa na Hamisa wakidai
sio mtoto wake.
Siku
ya jana Diamond aliachia trailer mpya ya shoo yake ya ‘The real Life of
Wasafi’ itakayoonyesha maisha halisi ya familia ya Diamond
itakayorushwa Kwenye Wasafi Tv.
Kwenye
trailer hiyo kuna kipande kinachomuonyesha Diamond akiwa anazungumzia
watoto wake lakini watoto wanaoonekana ni wawili tu ambao amezaa na Zari
huku mtoto wake aliyezaa na Hamisa hakuonekana.
Kuona
hivyo mashabiki wa Zari wakaanza kumnanga mtoto wa Hamisa kuwa sio
mtoto wa Diamond ndio maana hajaonekana kwenye trailer ya shoo ile na
hapendwi kama watoto wa Zari wanavyopendwa.
Baada
ya maneno mengi sana Diamond alishindwa kujizuia na kuandika kwenye
ukurasa wake wa Instagram kuwa Dylan ni mtoto wake kama walivyo watoto
aliozaa na Zari walionekana kwenye trailer ile sababu pekee ambayo
ilisababisha mpaka Dyalan hakuonekana ni kwa sababu hakuwa na clip yake:
Mpekuzi.
Comments