Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeitaka serikali kutoa maelezo ya
kina kuhusu watumishi wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuvamia Mgahawa wa
Bunge na kisha kuwapima samaki waliokuwa wakiuzwa, kitu ambacho
kinadaiwa haikuwa sahihi.
Kauli
hiyo imetolewa jana na Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson baada ya wabunge
kuomba muongozo wa kiti ili suala hilo lijadiliwe bungeni.
Akiomba
muongozo wa spika, mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba
kwa kutumia kanuni ya 47 alitaka bunge lisimamishe shughuli zake ili
kujadili jambo hilo.
Serukamba
alisema kuwa maofisa uvuvi walivamia Mgahawa wa Bunge bila kutoa
taarifa kwa Katibu wa Bunge, Spika wa Bunge wala Naibu Spika wa Bunge.
Aidha,
maofisa hao waliingia jikoni bila kufuata utaratibu wowote na kuvaa
vifaa mikononi na kuanza kupekua chakula ambacho tayari kilishapikwa,
jambo ambalo linatishia usalama wa wabunge.
Hata
hivyo, kutokana na hoja hiyo Naibu Spika wa Buge Dkt. Tulia Ackson
alikuabaliana na hoja ya mbunge huyo na kuitaka serikali leo itoe majibu
ya swala hilo.
Mpekuzi.
Comments