
Waziri huyo anatarajiwa kusoma bajeti hiyo, katika ukumbi wa Baraza
la Wawakilishi Mjini, ulioko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Akitoa muelekeo wa bajeri hapo juzi, Dk. Khalid alisema serikali
inakusudia kutumia shilingi trilioni 1.3, zikiwamo shilingi bilioni
807.5 zitazokuwa ni za vyanzo vya ndanina shilingi bilioni 464.2 kutoka
kwa washirika wa maendeleo.
Aidha alisema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mwaka huo wa fedha inatarajia kukua kwa uchumi wake kwa kasi ya 7.7.
Ofisa Uhusiano wa Baraza la Wawakilishi, Himidi Choko, alifahamisha
kuwa tayari maandalizi ya usomaji wa bajeti hiyo yamekamilika ndani ya
Baraza hilo ambapo wanatarajia kupokea wageni mbali mbali walioalikwa
katika taasisi tofauti.
Zanziba24.
Comments