Austria yataka kutumwa Afrika askari wa EU kuzuia wimbi la wakimbizi.

Austria yataka kutumwa Afrika askari wa EU kuzuia wimbi la wahajiri Waziri wa Ulinzi wa Austria, Mario Kunasek ametoa mwito wa kutumwa askari wa Gadi ya Mpakani ya Umoja wa Ulaya katika nchi za Afrika 'zinazoafiki pendekezo hilo' ili kukabiliana na wimbi la wakimbizi kutoka nchi hizo kueleke Ulaya.

Amesema Austria itashinikiza utekelezwaji wa mpango huo mara tu itakachopochukua uenyekiti wa EU kuanzia Julai Mosi.
Kauli hiyo ya Austria inatolewa katika hali ambayo, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wanakutana hii leo katika mkutano wa dharura mjini Brussels, kujadili jinamizi la wahajiri.
Nchi hizo za EU zimegawanyika kuhusu mbinu zinazopaswa kutumiwa na umoja huo kuzima wimbi la wahajiri wanaomiminika katika nchi za Ulaya, haswa wanaotokea nchi za Afrika.
Haya yanajiri siku chache baada ya kituo cha kutetea haki za binadamu Ulaya na Mediterania (EuroMed Rights) kutahadharisha kuhusu ongezeko la ukatili na vitendo vya kutumia mabavu dhidi ya wahajiri katika nchi za Ulaya na kuutaka Umoja wa Ulaya (EU) kukabiliana na ubaguzi barani humo.
Kituo hicho chenye makao yake mjini Geneva kimesisitiza kuwa, mbinu za kueneza chuki dhidi ya raia wa kigeni na ubaguzi dhidi ya wahajiri na wakimbizi ni pamoja na manyanyaso ya kimwili, kuchomwa moto kwa makusudi, mauaji, kuwazuia wakimbizi na wahajiri kutoka nje ya kambi zao, kuzuia mishahara ya wahajiri au kuwazuia kueleza utambulisho wao wa kidini kama vile vazi la hijabu la mwanamke wa Kiislamu. 
parstoday.

Comments