Ajali hiyo imetokea leo Juni 25 saa 10 alfajiri katika eneo la Dundani wilayani Mkuranga Mkoani Pwani.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Dk Stephen Mwandambo amethibitisha vifo hivyo, amesema maiti za watu 14 zimepokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.
"Ni kweli hili tukio limetokea alfajiri, tumepokea miili 14 na majeruhi wanne," amesema Dk Mwandambo.
Kati ya majeruhi hao, amesema mmoja hali yake ni mbaya na walikuwa wanahangaika kuokoa maisha yake.
Mwananchi.
Comments