
Halima Mdee ametoka kauli hiyo bungeni Mjini Dodoma, leo Mei 23, 2018
na kusema kuwa kuna walimu au watumishi wamelitumikia taifa hili kwa
miaka mingi sana, serikali inadhani ni sahihi kwa watumishi hao kuondoka
bila hata kifuta jasho?
“Zalio la vyeti feki ni Chama cha Mapinduzi na Serikali
yake, kwa kipindi hicho tunafahamu kwamba walimu au watumishi wengi
walianza na cheti cha mtu wakaenda wakasomea taaluma wakafaulu taaluma
zao wakaenda kulitumikia Taifa hili kwa miaka mingi sana, serikali ya
watu ni serikali yenye ubinadam mi nataka niulize swali la nyongeza hivi
kweli serikali ya CCM inadhani ni sahihi kwa watu ambao wametumikia
hili Taifa kwa miaka 20 wengine mpaka miaka 40 wengine hata miaka 30
waondoke hivi hivi bila hata kifuta jasho mnadhani ni sahihi.? amehoji Mdee.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Madini,Angellah Kairuki akijibu kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI amesema kuwa “Nafahamu
kuwa dada/Mdogo wangu naye ni mwanasheria ‘You can make benefit for
your own wrong’ suala hili lilikuwa ni jinai huwezi ukanufaika hata kama
uliweza kupenetrate katika mfumo ikafikiwa hapo na Ndio maana Mh. Rais
aliweza kutoa armnest na hii haikuweza kutoka bure, kwahiyo Mh. Halima
aweze kuelewa suala hili halijazalishwa na serikali ya CCM ni criminal
offence na ilikuwa ni lazima kufanya hivyo.”
Zanzibar24.
Comments